top
   
bunnertop
   


 

KAMPUNI YA BIA YA TANZANIA BREWERIES LIMITED YAANZA KUTUMIA BARCODES ZA TANZANIA


Afisa wa Tanzania Breweries Limited, Bw. Kilindu akiongea baada ya Kukabidhiwa mfano wa Barcodes ambazo zitatumika kwenye bidhaa za TBL, Kulia ni Mkurugenzi wa Masoko wa Wizara ya Viwanda na Biashara Bw. Odil Majengo

Kampuni ya Bia ya TBL imekuwa kampuni ya 127 kujiunga na mfumo wa ala za mistari yaani Barcodes za Tanzania.

Kwa kujiunga huko kunafanya jumla ya bidhaa zaidi ya 1800 ambazo ziko sokoni zinazotumia alama za mistari za Tanzania zinazotolewa na Kampuni ya GS1 (TZ) National Limited.
Awali kabla ya kujiunga na GS1 Tanzania, TBL walikuwa wakitumia alama za mistari toka GS1 South Afrika na hivyo bidhaa zao kuwa ana alama za mistari toka Afrika ya Kusini na Kenya.
Kampuni ya GS1 ambayo imeanzishwa kwa ushirikiano wa serikali na asasi za sekta binafsi ndiyo pekee yenye idhini ya kutoa alama hizo muhimu katika sekta ya uchumi na biashara nchini. Awali makampuni ya Tanzania yalikuwa yakipata huduma hizi toka nchi jirani ya Kenya na Afrika Kusini.

Kutokuwa na alama za mistari Nchi ilikuwa ikipoteza takwimu nyingi za kibiashara kwani ili uweze kuuza bidhaa zilizokamilika (Finished Products) kwenye soko la kimataifa ni lazima uwe na alama za mistari, kwa kutumia alama za nchi nyingine Tanzania ilikuwa inaongeza Takwimu za nchi nyingine kwenye takwimu za uchumi duniani na hivyo kuonekana inauza kidogo nje.
GS1 Tanzania ina miezi sita tangu ianze huduma zake nchini Tanzania na tayari makampuni ya kizalendo 127 yameshajiandikisha na huduma hii ikiwemo moja toka Demokrasia ya Kongo.
Kuna changamoto nyingi ambazo kampuni hii imekuwa ikikut na nazo kubwa ikiwa uelewa wa mfumo mzima na umuhimu wake hivyo elimu zaidi inabidi itolewe kwa wafanyabiashara na wajasiriamali wazalendo kuweza kujitokeza na kujiunga ili watumie alama hizi zinazotambulika na kukubalika kimataifa.

Changamoto nyingine ni kwa makampuni mengi makubwa kuendelea kutumia alama za mistari toka nchi za nje, GS1 imekuwa ikiendesha warsha mbali mbali na kuwatembelea wafanyabiashara na kuwaeleza umuhimu wa kutumia alama za mistari za Tanzania, Bado muitikio ni mdogo lakini tunaimani elimu imeanza kuwaingia na kwa makampuni makubwa kama TBL kurejea nyumbani kunaweza wavutia makampuni mengine kuja kutumia Barcodes za Tanzania.

Kwa upande wa Tanzania Mkoa wa Dar Es Salaam ndio unaongoza kwa wafanyabiashara wengi kujiunga na kuchukua Barcodes wakifuatiwa na mikoa Kilimanjaro na Arusha huku mikoa mingine kama Ruvuma, Rukwa ikiwa na takwimu ndogo sana za wafanyabishara kujiunga na mfumo huu.

 

 
 Map to GS1 (Click to zoom)

GS1 Live Chat
Form Object
 
 
All Rights Reserved |GS1 (TZ) NATIONAL LTD – Dar Es Salaam P.O. box 2476, Dar es salaam - Tanzania, Tel: +255 22 2150118, Fax: +255 22 2151016
Email: info@gs1-tanzania.org, Website: www.gs1-tanzania.org I Contact Webmaster