top
   
bunnertop
   


 

WAJASILIAMALI WAASWA KUSAJILI BIDHAA ZAO KWENYE MFUMO WA GS1 BARCODE


Afisa wa GS1 Pius Mikongoti, Akifafanua jambo kwa Waziri wa Viwanda na Biashara alipotembelea banda la GS1 kwenye maonyesho ya wajasiliamali wa Kanda ya Kaskazini yaliyofanyika kwenye viwanja vya Tangamano, Jijini Tanga hivi karibuni, Kulia ni Mkurugenzi wa SIDO Mark Laizer.

Wajasiliamali nchini wameaswa kusajili bidhaa zao kwenye mfumo wa utambuzi wa bidhaa wa Barcode unaotolewa na GS1 Tanzania. Hayo yamesemwa na Waziri wa Viwanda na Biashara Mheshimiwa Abdallah Kigoda alipokuwa kifungua rasmi maonyesho ya Wajasiliamali wa Kanda ya Kaskazini yaliyofanyika viwanja vya Tangamano Jijini Tanga hivi karibuni.

Mheshimiwa Kigoda alisema kuwa Serikali ilijua umuhimu wa mfumo huu kwa Taifa na ndio maana walibariki kuanzishwa kwake na kupitia wizara yake mfumo huu ukaanza rasmi mwaka jana hapa Tanzania.

"Nawaasa wajasiliamali kuutumia mfumo huu ili kuiwezesha pia serikali kujua na kufatilia kirahisi mauzo ya bidhaa zetu nje ya nchi, ikumbukwe kuwa ili uweze kuuza kwenye soko la ndani na la nje kwenye masoko rasmi ni lazima uwe na Barcodes kwenye bidhaa zako" aliongeza Mh Kigoda.

Mpaka sasa jumla ya makampuni 175 yamesajiliwa kwenye mfuomo huu huku kukiwa na bidhaa zaidi za 2500 ambazo zinatumia Barcodes za Tanzania zikiwa sokoni. Haya ni mafanikio makubwa kwa kipindi kifupi ambayo GS1 Tanzania imeyapata.

Bado juhudi na elimu inabidi itolewe kwa Watanzania wote ili nafasi na fursa hizi ziweze kufaidisha watanzania kwa ujumla.

Banda la GS1 Katika maonyesho ya SIDO Kanda ya Kaskazini.

 
 Map to GS1 (Click to zoom)

GS1 Live Chat
Form Object
 
 
All Rights Reserved |GS1 (TZ) NATIONAL LTD – Dar Es Salaam P.O. box 2476, Dar es salaam - Tanzania, Tel: +255 22 2150118, Fax: +255 22 2151016
Email: info@gs1-tanzania.org, Website: www.gs1-tanzania.org I Contact Webmaster