top
   
bunnertop
   


 

GS1 Yashiriki Maonyesho ya Nanenane Nzuguni Dodoma.


Afisa Muandamizi wa GS1 Tanzania Bw. Pius Mikongoti akitoa maelezo kwa mgeni rasmi Makamu wa Rais Zanzibar Balozi Seif Iddy baada ya kupita kwenye banda la GS1 kujua kuhusu huduma zitolewazo viwanjani hapo.

 

Taasisi ya GS1 Tanzania imeshiriki kwenye maonyesho yaliyoisha hivi karibuni ya Nanenane yaliyofanyika viwanja vya Nzuguni huko Dodoma. GS1 ilishiriki chini ya Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara ikiwa ni Taasisi inayojitegemea lakini inalelewa kwa kiasi kikubwa na Wizara.

Katika maonyesho hayo ambayo yalifunguliwa na Makamu wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Idd, GS1 ilikuwa ikitoa huduma ambapo makampuni ya wajasiliamali zaidi ya thelathini (30) yaliandikishwa yenye jumla ya bidhaa 82 zilipatiwa Barcode katika maonyesho hayo. Hii ni mara ya kwanza kwa GS1 kutembelea kanda ya kati, hivyo kulikuwa na changamoto nyingi kubwa ikiwa ni uelewa mdogo wa sio tu faida za Barcode bali huduma za GS1 kwa ujumla.

Maonyesho ya Nanenane yalifanyika kitaifa mkoani Dodoma huku mikoa mitatu ikishiriki kikamilifu nayo ni Dodoma, Singida na Tabora. GS1 iliwakilishwa na maofisa wawili Clemetina Kahamba na Pius Mikongoti ambao kwa pamoja walikuwa na jukumu la kutafuta wanachama wapya na kueleza umuhimu na faida za Barcode.

GS1 pia ilipata nafasi ya kutoa mada kwenye darasa ambalo liliandaliwa na Wizara ya Viwanda na Biashara ambapo jumla ya washiriki 246 walihudhuria kwenye siku mbili za vipindi vya GS1.

Clementina Gosbert (Membership Officer) akikagua moja kati ya bidhaa za wajasiriamali ambazo zina Barcode za Tanzania ili kuona kama zimewekwa sawa. Moja ya majukumu ya GS1 ni kuhakikisha Barcode zimekaa sawa kwenye bidhaa ikiwa ni pamoja na kuhakiki rangi zilizotumika, ukubwa na usahihi za namba, hii yote ni kuhakikisha Barcode zilizoko kwenye bidhaa zitasomwa na mashine kwa mara ya kwanza ziki skaniwa (first Scan, First read).

 
 Map to GS1 (Click to zoom)

GS1 Live Chat
Form Object
 
 
All Rights Reserved |GS1 (TZ) NATIONAL LTD – Dar Es Salaam P.O. box 2476, Dar es salaam - Tanzania, Tel: +255 22 2150118, Fax: +255 22 2151016
Email: info@gs1-tanzania.org, Website: www.gs1-tanzania.org I Contact Webmaster