top
   
bunnertop
   


 

LADY JAY DEE AWA MWANAMUZIKI WA KWANZA KUTUMIA BARCODES KWENYE ALBAMU YAKE MPYA  YA TANO.


Meneja wa Machozi Co. Ltd Gadna G. Habash akiwa ameshikilia CD ya Mwanamuziki Lady Jay Dee ambayo ina Barcode ya GS1. Lady Jay Dee anakuwa Mwanamuziki wa Kwanza kupata Barcodes.Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) Bw. Godfrey Simbeye.

 

Mwanamuziki Judith wambura Mbibo aka Lady Jay Dee amekuwa msanii wa kwanza kutumia Barcodes za Tanzania kwenye albamu yake mpya inayojulikana kama Ya 5. Toka kuanzishwa rasmi kwa shirika la GS1 (TZ) National Ltd hapa nchini takribani miezi sita iliyopita, shirika limekuwa likitoa barcodes kwa ajili ya bidhaa zote za wafanyabiashara mbali mbali hususani bidhaa za vyakula (Food processors), GS1 (TZ) National Ltd imeona ni wakati muafaka sasa kuanza kuwaangalia wasanii wanaotengeneza kazi zao hapa nchini kwa kuanza kutumia barcodes kama njia moja wapo ya kuwaandali soko rasmi (formalize) na kupanua soko hilo hadi kufikia viwango vya soko la kimataifa huko mbeleni. Kwa kuweka bar codes kwenye albamu/kazi ya msanii itawezesha albamu/kazi ya sanaa ya kitanzania kuweza kuuzika kwa kutumia teknolojia za kisasa za “scanner” katika point of sales (POS) na hivyo kuondoa utegemezi wa uzaji usio rasmi wa mitaani ambao hauwanufaishi wasanii wa kizi hizo hapa nchini.

Wasanii wamekuwa wakilalamika kuhusu kuwa na mfumo mzuri wa ufuatiliaji wa kazi zao kimasoko hivyo basi kwa kutumia Barcodes msanii kupitia meneja wake anaweza kupeleka kazi zake mwenyewe kwenye Supermarkets na kufuatilia mauzo bila kutumia mtu wa kati na hivyo kupunguza utegemezi wa wasambazaji wasio rasmi. Kwa kumpatia Lady Jay Dee Barcodes tunadhani huu utakuwa mwanzo mzuri kwa kushirikiana na BASATA na vyombo mbali mbali vinavyosimamia kazi na haki za wasanii kutengeneza mfumo wa ufuatiliaji kazi hizi kwa kutumia mfumo wa ufuatiliaji wa GS1 (Traceability) ili kupata ufumbuzi.

Taasisi ya GS1(TZ) NATIONAL LIMITED ni chombo kilichoanzishwa  kwa jitihada za wadau kupitia  Wizara ya Viwanda na Bishara na taasisi zake (BRELA, TIRDO, SIDO NA TANTRED) pamoja na  Taasisi za sekta binafsi nchini kupitia  ‘Tanzania Private Sector Foundation’ (TPSF).
Toka kuanza kutoa huduma hii ya Barcode nchini,  jumla ya viwanda/makampuni 127 yamekwisha patiwa Barcode zenye kiambishi “620” na jumla ya Barcode zaidi ya 1800 zimetolewa kwenye bidhaa mbali mbali hapa nchini. 
Kuna changamoto nyingi ambazo kampuni hii imekuwa ikikut na nazo kubwa ikiwa uelewa wa mfumo mzima na umuhimu wake hivyo elimu zaidi inabidi itolewe kwa wafanyabiashara na wajasiriamali wazalendo kuweza kujitokeza na kujiunga ili watumie alama hizi zinazotambulika na kukubalika kimataifa.

Changamoto nyingine ni kwa makampuni mengi makubwa kuendelea kutumia alama za mistari toka nchi za nje, GS1 imekuwa ikiendesha warsha mbali mbali na kuwatembelea wafanyabiashara na kuwaeleza umuhimu wa kutumia alama za mistari za Tanzania, Bado muitikio ni mdogo lakini tunaimani elimu imeanza kuwaingia na kwa makampuni makubwa kama TBL kurejea nyumbani kunaweza wavutia makampuni mengine kuja kutumia Barcodes za Tanzania.

Kwa upande wa Tanzania Mkoa wa Dar Es Salaam ndio unaongoza kwa wafanyabiashara wengi kujiunga na kuchukua Barcodes wakifuatiwa na mikoa Kilimanjaro na Arusha huku mikoa mingine kama Ruvuma, Rukwa ikiwa na takwimu ndogo sana za wafanyabishara kujiunga na mfumo huu.

 

 

 
 Map to GS1 (Click to zoom)

GS1 Live Chat
Form Object
 
 
All Rights Reserved |GS1 (TZ) NATIONAL LTD – Dar Es Salaam P.O. box 2476, Dar es salaam - Tanzania, Tel: +255 22 2150118, Fax: +255 22 2151016
Email: info@gs1-tanzania.org, Website: www.gs1-tanzania.org I Contact Webmaster