top
   

You are Here >> About Us

 

GS1 (TZ) NATIONAL LIMITED

TAARIFA  YA MWAKA  YA UTEKELEZAJI WA HUDUMA ZA GS1 (TZ) NATIONAL LIMITED  KUTOKA TAREHE 24 JANUARI 2011 HADI 24 JANUARI 2012 KWENYE MKUTANO MKUU WA WADAU UTAKAO FANYIKA KATIKA UKUMBI WA UBUNGO BLUE PEARL, DAR ES SALAAM  TEREHE 24 JANU ARI 2012

1.0 Utangulizi:
Kampuni ya GS1 (TZ) National Limited imeanzishwa kwa kusudio kubwa la kuweza kutoa huduma za Barcodes na teknologia nyingine zinazotewa na taasisi GS1 ulimwenguni, za kuendeleza biashara kimataifa na kitaifa. Imedhibitika kwamba chombo hiki, kabla ya kusajiliwa nchini,  wafanyabiashara wengi wa Tanzania walikuwa wakizifuata huduma za barcodes kutoka nchi za Kenya na Afrika ya Kusini. Chombo hiki kinasimamiwa na Mkutano Mkuu wa mwaka na Bodi ya Wakurugenzi.

Bodi ya GS1 (TZ) National Limited inapenda kuishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara pamoja na taasisi zake hususani TIRDO, SIDO, TANTRADE na BRELA kwa jitihada ilizozionesha katika usajili wa kampuni ya GS1 (TZ) NATIONAL LIMITED. Vile vile shukrani hizo pia zizifikie taasisi nyingine kutoka Sekta Binafsi kama TCCIA, TWCC, TPSF, TAHA, CTI, TEA ASSOCIATION OF TANZANIA, na ZNCCIA  kwa namna  zilivyoweza kuchangia katika zoezi zima la kuhakikisha taasisi  ya GS1(TZ) National Limited inaanzishwa na kusimama imara  kwa ajili ya maendeleo ya nchi  ya Tanzania.

Inafahamika kwamba miongoni mwa majukumu makubwa ambayo Wizara ya Viwanda na biashara inatekeleza moja wapo ya majukumu yake ni kuhakikisha kwamba sekta binafsi inasimama na inachangia katika pato la taifa. Bodi ya utawala ya GS1 (TZ) NATIONAL LIMITED inachukua fursa hii  kuipongeza Wizara ya Viwanda na Biashara  kwa kazi kubwa iliyo ifanya hadi taasisi hii ambayo itapunguza gharama za kuendesha biashara  nchini kuweza kuzaliwa. Kwa mantiki hiyo basi wafanyabiashara wa Tanzania  kwa sasa hawana sababu ya kununua Barcode kutoka katika nchi  za jirani kama Kenya na South Africa.

2.0 Historia fupi ya uanzishwaji wa GS1 (TZ) NATIONAL LIMITED
Kumbu kumbu, zinaonesha kuwa, Wizara ya Viwanda na Biashara kupitia shirika lake la  kuhudumia viwanda, TIRDO, walichukua jukumu, na kuishirikisha Sekta binafsi, chini ya mwavuli wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) na hivyo, kuweza kuunda sekretariate ambayo, chini ya uwenyekiti wa Ndugu Adamu Zuku, kazi kubwa ilifanyika na chomboa hiki kikaundwa. Wajumbe wa Secretariat ambao walikutana kwa takribani miaka miwili  waliwezesha kuundwa kwa chombo hiki ni  wafuatao:

Idadi

Wajumbe

Taasisi walizowakilisha

1.

Bi. Jacqline Maleko

Wizara ya Viwanda  na Biashara

2.

Bw. Elibariki Shami

Wizara ya Viwanda  na Biashara.

3.

Bi. Magdalena Hall

Wizara ya Viwanda Biashara na Masoko

 4.

Bi. Adamu Zuku

Tanzania Chambers of Commerce Industries and  Agriculture

5.

Bw. Andrew Mphuru

Tanzania Private Sector Foundation

6.

Bw. Hans Mtika

Tanzania Private Sector Foundation

7.

Bi. Fatuma Kange

Tanzania Private Sector Foundation

8.

Bw. Ignas Mganga

Confederation of Tanzania Industries

9.

Bw. Louis Accaro

Tanzania  Private Sector Foundation

10.

Bi. Fatuma  Ryiami

TAHA/ Nature Ripe

11.

Bw. Anselm Moshi

TIRDO

12.

Bi. Purification Andrew

TIRDO

13.

Bw. Humphrey Ndosi

TIRDO

14.

Bw. Hussein Komte

Confederation of Tanzania Industries.

15.

Bw. Ignasi Mganga

Confederation of Tanzania Industries

16.

Bw. Khamis Issa Mohamed

ZNCCA

17.

Bw. Ayoub Sykes

Digiscan

18.

Bw. Geoffrey T. Mbaga

TCCI Morogoro

19.

Bi. Dina Bina

Women Chambers Of Commerce.

21.

Dkt . Manenge L.C

TIRDO

22.

Dkt . Asifa Nanyaro

TIRDO

23

Bw. Jones M. Sikira

Tea Association

 

2.1 Mambo ya kuzingatia katika kuunda chombo kitakacho simamia huduma za GS1  katika nchi yoyote

 • Lazima chombo cha kuendesha huduma za GS1 nchini kipatikane kwa njia ya haki na uwazi na kishirikishe wadau mbalimbali kwa kufanya uchaguzi wa mkutano mkuu.(Kwa maana ya wale waliojaza “Endorsement Letter”
 • Mchakato wa uanzishwaji wapaswa kuwahusisha walaji, wazalishaji watumiaji wa bidhaa na wasambazaji  wa  maduka makubwa kama (Supermarkets)
 • Lazima kisimamiwe na bodi ya utawala “Management Board” na bodi hii ni lazima itokane na Mkutano Mkuu ambao utaichagua “Wajumbe wa Bodi” ambao watasimamia kampuni  katika nchi husika, ambao wataajiri Mtendaji Mkuu wa kuendesha shughuli za kila siku za chama.
 • Kampuni itakayofunguliwa iwe  ni kampuni isiyotengeneza faida yaani “Non Profit making company”.

 Nchini Tanzania, baada ya kila kitu kufanyika, kwa maana ya kuwa na idadi ya wanachama mia mbili na hamsini (250) waliojaza “endorsement letters”, na kuwa na “Business Plan”, Hatua iliyofuata ilikuwa ni kuitisha Mkutano Mkuu wa wanachama waanzilishi ili kupata “Bodi ya Utawala” mkutano mkuu ulifanyika tarehe 24/01/2011 katika hoteli ya Blue Pearl. Mkutano huu ulihudhuriwa na wajumbe kutoka Zanzibar na mikoa mbalimbali  ya Tanzania bara

  • UCHAGUZI WA BODI YA UTAWALA:

Uchaguzi ulikuwa wa huru  na wa haki , ambao wajumbe mbalimbali walijitokeza katika  kuomba kura mbele ya  wanachama zaidi ya mia mbili na hamsini waliohudhuria mkutano ule. Hivyo hadi tunafika mwisho wajumbe wafuatoa ndio waliochaguliwa kuwa wajumbe wa bodi:-

Idadi

Majina

Nafasi

1.

Elibariki Mmari

Mwenyekiti

2.

Yakub Hasham

Makamu Mwenyekiti

3.

Esther Mkwizu

Mjumbe

4.

Khamis Issa Mohamed

Mjumbe(Zanzibar)

5.

Dina P. Bina

Mjumbe

6.

Dr. Gideon W. Mazara

Mjumbe

7.

Mathews Kaubo
SHOPRITE Tanzania

Mjumbe

8.

Leopard Lema
Manufacture of fruit Wine

Mjumbe

9.

Hanry Mashinga
RETAIL Distribution
IMALASEKO

Mjumbe

10.

Adamu Zuku

Mjumbe

11.

Fatuma Ryiami

Mjumbe

3.0 Usajili:
Kampuni hii ya GS1  (TZ) NATIONAL LIMITED ilianza kazi zake mara baada ya kupata usajili. Usajili wa kampuni hii ulifayika baada ya Mkutano Mkuu uliofanyika tarehe 24/Januari/2011 katika ukumbi wa mikutano wa  Hoteli ya Ubungo Blue Pearl iliyopo Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wanachama waanzilishi zaidi ya 250. Mgeni rasmi katika Mkutano wa kwanza alikuwa Mh. Waziri wa Viwanda Bw. Cyril Chami ambaye aliwakilishwa na Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda Hon. Joyce Mapunjo  wa wadau ailikuwa ni Mh. Joyce Mapunjo. Usajili wa kampuni hii ukafanyika tarehe 28. 02.2011 katika taasisi ya usajili wa makampuni ya BRELA. Baada ya  usajili kufanyika, na kulingana na taratibu na kanuni za usajili nchini Ubelgiji, hatua iliyofuata ilikuwa ni kutuma maombi ya kusajili kwa kampuni hii nchini ubeligiji ikiwa na viambatanishi vifuatavyo:-

 • Idadi ya majina ya wanachama waanzilishi
 • Mchanganuo wa Biashara (Business Plan)
 • Cheti cha Usajili
 • Barua ya kuitambua GS1 (TZ) National limited kutoka Serikalini  na viambatanisho vingine muhimu.

Baada ya maombi haya kutumwa  hatimaye mnamo tarehe 18 Mei 2011 kupitia Mkutano Mkuu wa wanachama uliofanyika nchini Ufaransa katika mji wa Paris kwenye Hotel ya Marriot River Gauche,  kampuni ya  GS1 (TZ) National Limited  iliwezakupata usajili wa kudumu na hivyo nchi yetu iliingia kwenye rekodi kwa kuwa ni mwanachama namba 109 na kukabidhiwa  namba kiambishi (Prefix No) 620.

4.0 Ofisi za GS1 (TZ) NATIONAL LIMITED
 
Kwa sasa ofisi za GS1 (TZ) National Limited zipo katika ofisi za SIDO zilizopo katika Mtaa wa Ufaume Upanga jijini Dar Es Salaam. Ofisi hizi zimeajiri wataalamu sita ambao wanaweza kuendesha kutoa huduma za GS1 nchini.

5.0 Mafunzo
Ili kuwapa uwezo watendaji wa GS1 (TZ) National Limited,  mafunzo ya namna ya kuendesha technologia hizi yalifanyika na wataalamu wakapewa mbinu mbalimbali za namna ya kutoa Barcodes, umuhimu wa Barcodes katika biashara za kila siku. Mafunzo hayo yalidhaminiwa na Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF). Mtaalamu muwezeshaji na mshauri  ailikuwa ni ndugu Joseph Nyongesa kutoka nchini Kenya. Mafunzo hayo pia yaliweza kufanyika kwa wafanyabishara, wafanyakazi wa serikali pamoja na Bodi ya GS1 (TZ) National Limited. Muda wa mafunzo hayo ulikuwa wa wiki mbili.

 

5.1 Utoaji wa huduma za barcodes
kuanza kutoa huduma za utoaji barcode kuliwezeshwa kwa kiasi kikubwa na serikali baada ya kutupatia, vitendea kazi muhimu ambavyo ni computer moja ya mezani, photocopier moja na barcode printer. Kwa mantiki hiyo mnamo tarehe hiyo 23/8/2011 mteja wa kwanza kwa kutoka nchini  aliweza kupata BARCODE yake kutoka katika kampuni yetu. mteja huyu ni Masasai Food  Industries Company Limited kutoka kibaha pwani.  utoaji wa barcode hii ya kwanza  uliweza kufanikishwa kwa kiasi kikubwa kutoka kwa muwezeshaji kutoka kenya mr. joseph nyongesa ambaye amedumu katika utoaji wa huduma za GS1 nchini kenya kwa miaka mingi. siku hiyo ilikuwa ni siku ya faraja sana kwa wafanyakazi wa GS1 (TZ) NATIONAL LIMITED, na bodi yote.

6.0 Idadi ya wanachama
Kwa ujumla ukitaka kuangali idadi ya wanachama wa GSI (TZ) National Limited ni lazima kwanza uzingatie  wanachama waanzilishi ambao, kupitia mkutano mkuu wa wanachama uliofanyika tarehe 24. 01. 2011 katika ukumbi wa Ubungo Blue Pearl wakati wa kuchagua GSI (TZ) National Management Board walikuwa 257. Kwa mantiki hiyo basi, baada ya kuanza kutoa huduma za GSI idadi ambayo tumeshawapatia  barcode hadi sasa ni wanachama zaidi ya 92. Uzoefu umetuonesha kwamba panapotekea maonesho na GS1 kushiriki habari zimeweza kuwafikia watu wengi kwa wingi na hivyo, kuweza kujitokeza na kupatiwa huduma za Barcodes nchini.

Hadi sasa kwa twakwimu zetu, sekta ya  usindikaji ndiyo imejitokeza kuchukua barcodes nyingi ukizilinganisha na nyingine. Bado uhamasishaji unahitajika ili huduma yetu zifikie sekta nyingi zaidi.

 

Hadi sasa kwa twakwimu zetu, sekta ya  usindikaji ndiyo imejitokeza kuchukua barcodes nyingi ukizilinganisha na nyingine. Bado uhamasishaji unahitajika ili huduma yetu zifikie sekta nyingi zaidi.

Mpaka leo tarehe 19/01/2012 taasisi yetu ina jumla ya wanachama zaidi ya tisini na mbili (92) ambao kwa ujumla wao wanafanya idadi ya bidhaa zenye Barcode ya Tanzania kuwa zaidi ya 1,300 ambazo ziko sokoni.  Juhudi kubwa zinaendelea kufanyika ili  kuyatembelea makampuni makubwa ambayo yalikuwa yakitumia Barcode za nje ya nchi ili waweze kuhamia kwenye Prefix ya Tanzania na mengi ya makampuni hayo yameanza kuonesha nia ikiwano Tanzania Breweries Ltd. (TBL) na A to Z

 

Uchukuaji wa barcode wa mikoa

Hadi sasa kuna mikoa ambayo haina hata majasiriamali ambaye ameshasajili na GS1 (TZ) National Limited ili kukupata Barcodes. Kazi bado ni kubwa na uhamasishaji unahitaji kwa kiasi kikubwa

 

7.0 Ada
ili kuweza kuendesha  leseni ya GS1 ya dunia ni wajibu kwa wanachama wa GS1 katika nchi husika kuweka viwango vya ada ili kuweza kulipia leseni kwa mwaka. kwa mantiki hiyo basi, viwango ambavyo vinatumika katika kuendesha shughuli mbalimbali za gs1 ni kama vifuatavyo:-

 

Annual Turnover Amount

Registration Fee
(Paid only Once)

Annual License Fee

Category 1:

Start up             to       Tshs  10M

100,000/=

       100,000/=

Category 2:

Tshs 10.1M       to       Tshs  40M

 100,000/=

    200,000/=

Category 3:

Tshs 40.1M       to       Tshs  80M

 100,000/=

    400,000/=

Category 4:

Tshs 80.1M       to       Tshs  200M

               100,000/=

    1,300,000/=

Category 5:

Tshs 200.1M      to      Tshs  500M

 100,000/=

   2,000,000/=

Category 6:

Tshs 500.1 and above

 100,000/=

    2,640,000/=

Service providers

 

 100,000/=

    2,640,000/=

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Uchukuaji wa barcode kwa kuangalia gharama

Uchukuaji wa barcodes kulingana na category (kwa asilimia)

Hadi sasa, ukiangali viwanda vikubwa idadi yao ni ndogo ikilinganishwa na wale wajasiriamali wadogo ambao wengi ndio wamehamasika. 51% imechukuliwa na category ile ya ndogo ililinganishwa na 2% ya viwanda vikubwa.

 

8.0 Uhamasishaji:

Ingawa taasisi hii ya GS1 (TZ) National Limited bado ni changa sana, na bado inakabiliwa na uhaba wa fedha, ila imeweza kwa kushirikiana na Tanzania Private Sector Foundationa (TPSF) kuweza kutoa mafunzo ya uhamasishaji katika kanda mbili nchini. Kanda ya Ziwa, mafunzo yalifanyika tarehe 17th hadi 19 October 2011 katika hoteli ya Mwanza Hoteli  wakati Kanda ya Kaskazini mafunzo yalifanyika tarehe 24 hadi 27 October 2011, katika hoteli ya SG Hoteli.

Wafanyakazi wa GS1 (TZ) National Limited kwa vipindi mbalimbali wameweza kuongea na vyombo vya habari vikiwemo radio na Television na Magazeti katika hali ya kujitangaza. Hata hivyo jitihada mbalimbali za kuongeza uhamashaji inabidi ziongezwe  ili huduma hii iweze kuwafikia wazalishaji wengi zaidi.

8.1 Uzinduzi:
Mara baada ya usaji wa kudumu kupatikana, kilichofuata ulifanyika uzinduzi, wa kampuni ya GS1 (TZ) National Limited nchini ambayo, ni katika sehemu ya kujitangaza, ambapo uzinduzi huo, ulifanyika kipindi cha Sabasaba mwaka jana tarehe 4th Julai 2011 na Mh. Makamu wa Raisi, ndugu Ghalib Bilali.

 

 

 

8.2 Press Conference
ilifanyika tarehe,  ambayo ilikuwa na jukumu za kutangaza mwanzo wa kuanza kuhuduma za GS1 nchini. Press Conference ilishirikisha vyombo mbalimbali vya habari ambavyo ni Magazeti, Tv, Radio na Blogs.

 

8.3 Tovuti
Tovuti ya GS1 (TZ) National Limited imeshatengenezwa ambapo, kazi, wajibu na report mbalimbali zitakua zinatolewa kupitia tovuti hii www.gs1tz.org Tovuti hii pia itazinduliwa Leo tarehe 24/1/2012 kwenye Mkutano mkuu wa Wadau wa GS1 (TZ) National Limited. Vilevile kwenye facebook www.facebook.com/gs1tz account, ambayo imetegenezwa zaidi ili kuwa karinu na wateja wa GS1 (TZ) National Limited.

9.0 Changamoto:

 • Uhaba wa fedha wa kufanyia kazi. Tuna changamoto kubwa sana ya kifedha ili tuweze kujiendesha hasa kuweza kufanya “Promotion” ya ulewa juu ya huduma za GS1 na Barcode katika maendeleo ya nchi. Gs1 ni taasisi  mpya nchini basi haina budi kujitangaza kwa nguvu sana ili tuweze kuona lengo linafikiwa. Watanzania walio wengi wajiasiriamali na hata wafanya biashara wakubwa wote kwa pamoja hawajui uwepo wa huduma hizi nchini wala umuhimu na manufaa ya huduma hizi za barcodes katika bidhaa na nchi yao. Kwa kujua hilo, hawa wote wanatakiwa wapewe elimu ya barcode na huduma nyingine zitolewazo na GS1 na manufaa yake kwao binafsi na hata kwa nchi yetu kwa ujumla.
 • ushirikiano. changamoto nyingine kubwa ni ushirikiano mdogo ambao tunapata kutoka kwa makampuni mengi makubwa yanayopatikana hapa nchini ukilinganisha na ushirikianao mkubwa tunaopata kutoka kwa wajasiriamali  wadogo wadogo. kwa kweli muitikio wa haya makampuni makubwa kwa tanzania umekuwa ni mdogo sana ukilinganisha na tulivyodhani kwamba haya makubwa ndio yatakuwa na muitikio mkubwa sana kuliko wajasiliamari wadogowadgo. ukiangalia wanachama waliowengi katika taasisi yetu ni smes ukienda kwa makampuni makubwa tunapata majibu yasiyoridhisha hasa kwenye upande wa bei (wanataka kulipa bei sawa na mtu anayetengeneza achali au mbilimbi kwa makusanyo ya ndani ya milioni kumi kwa mwaka). Ukilinganisha na nchi nyingine ambazo wanatoa hizo barcodes tanzania ndio nchi tunayo lipisha gharama chini.

 

MAPENDEKEZO:

 • Tunaomba Wizara ya Viwanda na Biashara  kusaidi katika suala la “promotion” kupitia miradi mbalimbali amabayo wanaiendesha. Vilevile kusaidia kaiwezesha kampuni hii, katika kutoa Mafunzo juu ya mfumo wa Barcodes kwa Kanda zote nchini. Mafunzo haya hatasaidia katika kuongeza watumiaji wa Barcodes nchini. 
 • Kuiwesha GSI kuweza kuyafikia makampuni mbalimbali nchini kuweza kutumia mfumo wa ufuatiliaji wa Barcodes na kurahisha katika kuongeza ufanisi, kama : TRA, TCRA, TBS, TFDA, nk.

 

 • Kushirikiana na Wizara katika kundaa semina mbalimbali katika ngazi za mikoa na wilaya ili kuweza kuwafikia wajasiriamali wengi zaidi.
 • Kutengeneza Task force ya kitaifa itakayokuwa  kwa kushirikiana na ofisi ya gsi kuweza kuipenyeza huduma hii gsi  katika ngazi mbalimbali  za kiuchumi ili kuweza kuongeza pato la taifa.

 

 • Upatikanaji wa vifaa mbalimbali vya ofisi kama madawati au meza za kufanyia kaz, computer, laptop na viti vya wateja
 • Kuisaidia GS1 (TZ) National Limited kutengeza Strategic Plan, ili iweze kutekeza kazi zake kwa mikakati endelevu.

MAKAMPUNI AMBAYO YAMEKWISHA SAJILIWA NA GS1 (TZ) NATIONAL LTD

MM NO.

COMPANY NAME

REGION

CONTACT PERSON

1

GLOBAL LEATHER CENTER LTD

MWANZA

MR. E. N. MMARI

2

MASASI FOOD IND. CO. LTD

PWANI

 

3

FIVESTAR LTD

DSM

ASHIK ABBAS KARIM

4

NATURERIPE KILIMANJARO LTD

DSM

FATMA RIYAMI

5

NAMBUA ENTERPRISES

DSM

HELEN MWAMKOA

6

KWENMILL ENTERPRISES

MOSHI

ELIA SIFIWE ZAKARIA

7

TAZOP LTD

DSM

KHAMIS ISSA MOHAMED

8

MOUNTAIN GREEN

ARUSHA

EPHATHA N. S. NNKOH

9

MWANZA QUALITY WINES

MWANZA

LEOPORD LEMA

10

TROPIX HONEY

DSM

MRS EDNA MBAGA

11

AFRICAN STANDARDS & TELECOMMUNICATION LTD

DSM

SALMA K. MIRAJI

12

HONEY CARE AFRICA (T) LTD

DSM

JAYEN

14

APECHA BUSNESS  CONSALT LTD

DSM

PETER CHAMI

15

TUSAJIGWE G&FOOD SUPPLIES

DSM

MWL.ROSE ROMANUS

16

SINDIMBA CASHEWS LTD

DSM

MANU GUPTA

17

MAM CASHEWNUT REVOLUTION

DSM

MARIAM MAJID

18

NRONGA WOMEN DAIRY       CO-0PERATIVE SOCIETY

MOSHI

HELLEN USIRI

19

KIJIMO DAIRY CO-OPERATIVE

MOSHI

MAGRETH SIRIKWA

20

HAPPY FOOD TABATA

D'SALAAM

 

21

MWENGE WINE PROCESSORS

K'NJARO

DORICE KISSE MSUYA

22

SEFRA PRODUCT

 

 

23

KENI MODERN WINE

ARUSHA

ANTIPAS JOSEPH SHAO

24

JALI NATURAL PRODUCT

ARUSHA

JAMES DAMIAN NKANGHAA

25

TURIM FOOD PRODUCT

PWANI

MULIBAKE MWANGALABA

26

FAMA FOODS PROCESSING

IRINGA

GENOVEFA BARNABAS

27

AGATHA FOOD PROCESSOR

D'SALAAM

AGATHA SAIMON MHOJA

28

KALALI WOMEN DAIRY COOPERATIVE SOCIETY LTD

MOSHI

NANCY KIDIN

29

CHOICE COFFEE CO. LTD

MOSHI

ROSE ALEONASAA SWAI

30

MELISE ENTREPRISE GROUP

PWANI

ANNA KAFURU MWAKIHABA

31

SINGIDA FRESH OIL MILL

SINGIDA

ABDALLAH ALLY OMARY

32

EQUATOR NATURAL COSMETICS

D'SALAAM

Anna B.Mnaya(Mrs)

33

RELIM COMPANY LTD

D'SALAAM

MS RITHA MWAMANGA

34

AMBONI BEACH LTD

TANGA

STEVE KABWOYA

35

BAOBAB FRUIT COMPANY

DODOMA

ALEX RICHARD UROKI

36

KASULU BEEKEPERS CO-OP SOCIETY

KIGOMA

STAFORD E. M. NKUBHAGHANA

37

K'S ENTERPRISES LTD

MOSHI

ALEX INDEHORIO

38

G. E.M NATURAL FOODS

D'SALAAM

ZEBIDA G. MBWAMBO

39

KATANGA OIL REFINERY S. P. R. L.

LUBUMBASHI

AHMED ABBAS RASHID

40

AKTZ INDUSTRIES LTD

D'SALAAM

INNOCENT LUGHA BASH

41

BEST ANIMAL FEED LIMITED

D'SALAAM

TUMSIFU STEPHEN

42

SMOKE HOUSE STORE

D'SALAAM

TEDDY A DAVIS

43

HANN FOOD PRODUCTS

PWANI

COSTANCIA SOLOMONI

44

NDULA PRODUCTS

D'SALAAM

JANET MLOWE

45

MED-FOODS ARUSHA

D'SALAAM

JOYCE JOSEPH MMARI

46

EURO CONSULTANCY LTD

D'SALAAM

DISMAS L. MASSAWE

47

PROFATE INVESTMENT

D'SALAAM

FEDDY P. TESHA

48

BK TEA BLENDERS LTD

KAGERA

Dr PETTER A. MGIMBI

49

FRABHO ENTERPRISES LTD

D'SALAAM

JULIUS WAMBURA

50

BETTER LIVING ADVOCATES

D'SALAAM

TENGA B. TENGA

51

B CAKES CONFECTIONARY

MOSHI

THERESIA E. LASWAI

52

MLAKO PURIFIED ICE CUBES LTD

D'SALAAM

JOSEPH M. MLAY

53

KISHENGA ENTERPRISES

D'SALAAM

ANNA KIMAMBO

54

DM FASHION

D'SALAAM

EDNA ONAI

55

HACHAJE PRODUCTS

KILIMANJARO

HAIKASIA CHAKI

56

ESTER GILBERT BGOYA

KILIMANJARO

ESTER GILBERT

57

TANGA PHARMACEUTICALS & PLASTICS LTD

TANGA

AHMEDIRFAN M. HASSANALI

58

JAGEF GROUP

KILIMANJARO

ESTHER  A.MOSHI

59

JEAMS'S PRODUCTION

RUVUMA

MAGDALENA A.TARIMO

60

TABISCO ENTERPRISES

D'SALAAM

V. KUTUMBALAO

61

MAKINI BOTANICAL PRODUCTS

MBEYA

 

62

UNYANYEMBE  TRADERS LTD

TABORA

GEORGE JACKSON

63

EDGEWOOD INVESTMENTS PRIVATE LTD.

D'SALAAM

ALOYCE E. MASAWE

64

A3N PUBLISHER

D'SALAAM

AMON B. SWAI

65

MEGATRADE INVESTMENT LIMITED

ARUSHA

HAPINESS KIMARO

67

JUDITH CASHEWNUTS PAC..

D'SALAAM

JUDITH PETRO

68

ARUSHA WOMEN ENTREPRENEUR

ARUSHA

DAVID E. MUJUNI

69

TURU TRAIDING CO LTD

SINGIDA

ISSA MSOMA

70

BOMALANG'OMBE VILLAGE CO.

IRINGA

VIRGILIO KIHWELE

71

MAMASALT GROUP CO.

PWANI

YAHYA HASSAN

72

FEBENASHA GENERAL COMPANY

D'SALAAM

FELIX W. NKYA

73

JACKMA J. ENTERPRISES

DODOMA

JACKSON A. MASAWE

74

AROE NUTRI FOODS

IRINGA

ROSEMARY STAKI

75

RACHEL M NDYETABULA

D'SALAAM

RACHEL M. NDYETABULA

76

VIWIGO AGRO PROCESSOR ENTE

ARUSHA

WILLIAM SWAI

77

IKUWO GENERAL ENTERPRISES

MTWARA

SADRUCK ENOCK

78

HARMAH TRADERS &C0 LTD

D'SALAAM

JUMA ABASS

79

KANGARUU BRANDS

ARUSHA

 

80

S.F KHAMIS TRADERS

DSM

 

81

FOOT LOOSE TANZANIA LTD

DSM

 

82

CRM INVESTMENT LTD

DSM

 

83

ALLIED CHEMICALS LIMITED

 

 

84

IGOMBELO GROUP

DODOMA

 

85

GRAND CONFECTIONARY BAKERY LTD

DSM

 

86

Mek One General Traders Co. Ltd

87

MUSOMA FOOD COMPANY LIMITED

MUSOMA

88

CONQUERORS INTERNATIONAL WG LTD.

89

BEST ONE

90

BHUNU MBUNDI COMPANY LIMITED

91

ROYAL HONEY CO. LTD

92

Eliesh Group

 

 

Imetolewa:
GS1 (TZ) Management Board

 

 

 

 
 
All Rights Reserved |GS1 (TZ) NATIONAL LTD – Dar Es Salaam Tel: +255 22 2851007, Email: dcfr@cfr.ac.tz , Last Update: 24 May 2011 Powered by P-Informatics Co.Ltd